"Marehemu namfahamu, Mbalu Yabisa, alikuwa dada yangu. -- - Mnamo mwaka 1982 --- mtoto wangu aitwae Luja d/o Kasongi alianguka ndani ya lambo akafa. Nilienda kwa wanganga wa kienjeji baada ya mazishi. Waganga wa kienyeji walinieleza kwamba binti yangu Luja akisukumizwa kwenye lambo na akafa. Mnamo mwaka 1983 --- mtoto wangu wa kiume aitwae John Kasongi nilikuta analia naye akanieleza kuwa ametishiwa na shangazi yake (marehemu). Wakati huo alikuwa amechomwa na mwiba wa Mkongo (goti) nilimpeleka hospital --- nwisho akapona lakini shangazi yake hakuja kumtazama. Baada ya kuona kuwa anataka kumaliza watoto wangu nikajua kuwa siku moja ataniua mimi. --- Hivyo niliona kuwa nihame. Baada ya kuhama ndipo niliamua nimuue mimi mwenyewe. Mnamo tarehe 15 October 1984 saa 8 usiku niliondoka kwangu nilipofika kwa marehemu nilifungua mlango, nilimkuta amelala nilimvuluta toka kitandani nikamsukuma akajipiga kwenye kibambaza na kuanguka chini ndipo nikaanza kumniga kooni kwa mikono mpaka akafa. Baada ya kuona kuwa amekufa nilimvuta nikampeleka nadani ya choo; baada ya kuutumbukiza ndani ya choo nilichukua jembe nikaufunika kwa udongo --- nilipomaliza nilienda nyumbani kwangu."